Wednesday, 16 March 2016

MPENDE MWANAMKE WAKO!


Kila mwanaume ni bora akasoma hii.
Mpende mwanamke wako... 
Anapoonja kahawa, chai au chakula anajaribu kama kweli kinakufaa wewe mfalme wake.
Mpende mwanamke wako.. 
Pale anapokukumbusha kuswali. Anataka kuwa na wewe katika ufalme wa Mungu hapo baadae.
Mpende mwanamke wako..
Pale anapokukumbusha kusali pamoja na watoto wenu hataki kufanya aonekane watoto ni wamama pekee bali ni wa baba na mama.
Mpende mwanamke wako...
Pale anapokua na wivu na wewe nje ya wanaume wote ambao kimsingi angeweza kuwa nao ila amejitoa kwako na kuolewa na wewe.
Mpende mwanamke wako....
Pale anapokuomba umsaidie kuwaelekeza watoto homework zao. Anachotaka ni wewe kuwa sehemu ya familia.
Mpende mwanamke wako...
Pale anapoonekana ni mrembo na amependeza, ni wako mkubali na ujivunie kuwa na yeye.
Mpende mwanamke wako...
Pale anapotumia muda mrefu kujiremba wakati wa mtoko wenu, anachotaka yeye ni kuonekana anavutia ili asikuaibishe mbele ya jamaa na marafiki.
Mpende mwanamke wako...
Pale anapokununulia zawadi ambayo kimsingi haujaipenda, tabasamu na umwambie kwamba hicho ndicho siku zote ulikua ukikihitaji.
Mpende mwanamke wako... 
Pale anapolia pasina kujua sababu ni nini wewe mkumbatie, mfariji na kumwambia kila kitu kitakuja kuwa sawa.
Mpende mwanamke wako...
Pale anapokueleza njia sahihi za kuendesha gari, anachotaka yeye ni wewe kuwa salama siku zote.
Mpende mwanamke wako...
Yeye ni wako, mwanamke ni sehemu ya maisha yako anatakiwa atunzwe kama malkia. Wanaume bora kabisa ni wale ambao wanawatunza wake zao pasina misuguano ya aina yeyote ile!
Wanaume mmenisikia??
Share it, Like it.
Tweve
Loyan!

0 comments:

Post a Comment