Si ngumu kama unavyofikiri kuharibu kwenye usaili wa kazi.
Wasiwasi ambao hutokea pindi unapokaa upande wa pili wa mtu anayekufanyia usaili na kujikuta unalazimika uongee ili ukubalike na kupatiwa kazi mara nyingine inasababisha useme jambo ambalo hukulikusudia.
Hilo linaeleweka sana, lakini ni kauli gani zinaweza kukukosesha kazi?
1. ‘Niliacha kazi yangu kwa sababu mazingira hayakuwa mazuri/bosi wangu alikuwa mkorofi sana’
Usilalamike kuhusu kazi yako/bosi wako wa sasa. Kila muajiri anahitaji watu wenye mtazamo chanya, na huwa inawashtua sana kama mtu anayefanyiwa usaili anakuwa mkosoaji sana.
Kulalamika kuhusu mabosi wako waliopita ni miongoni mwa vitu vibaya zaidi kufanya kwenye usaili wako. Waajiri wengi wanaisema hii kuwa ni sababu kubwa ya wao kuwaacha watu wengi wanaojitokeza kuomba nafasi mbalimbali za kazi.
Kama ilivyo katika mahusiano ya kimapenzi, unapokutana na mtu kwa mara ya kwanza, unajaribu kuona kama kuna viashiria vibaya kutoka kwake. Jaribu kuepuka visionekane kwako kwa namna yoyote ile uwezayo. Kimsingi, hakuna anayependa mtu wa kulalamika sana.
Kuiongelea vibaya kazi uliyonayo sasa inaashiria hatari kwa anayekufanyia usaili kwamba yawezekana ukawa mkorofi kazini, au kwamba wewe ni mtu unayependa kuulaumu uongozi kwa makosa yako ya kutofanya kazi vizuri. Na kwamba baada ya muda mfupi utafanya usaili sehemu nyengine na utaongea hivyo kuhusu wao.
2. ‘Nimekuwa nikihama hama kazi kwakuwa sijapata sehemu sahihi bado/sijapata changamoto za kutosha
Kauli kama hii ni rahisi kuonesha kuwa huna malengo maishani mwako na itamfanya anayekusaili kuwaza: ‘Nafasi hii anayoitaka itakuwa na tofauti gani? Bila shaka atataka kuondoka baada ya miezi sita tu. Muajiri anahitaji mtu anayeweza kuwa naye kwa muda mrefu na anayeweza kuifanya kampuni ikue kwa kuleta mawazo mapya na kutafuta suluhisho kwenye changamoto zitakazojitokeza.
3. ‘Kampuni yako inahusika na nini/makao makuu ni wapi?’
Hii ni kanuni ya jumla ya kuzingatia unapokuwa kwenye usaili wa kazi: kama swali lako linaweza kujibiwa kwa kutafuta kwenye Google, basi usiliulize.
Unatakiwa kufanya utafiti wa kutosha mapema kabla ya kwenda kwenye usaili. Usiulize ‘maswali ya kawaida’ kuhusu kampuni unayoiomba kazi. Ni muhimu sana kujiandaa na uandae maswali yako yaweze kukupa majibu ya ndani. Kama utajiandaa vyema, muajiri atavutiwa zaidi nawe na usaili wako utakuwa na maana zaidi.
5. ‘Kama meneja, huwa nafanya kazi peke yangu zaidi’
Kama mnazungumzia nafasi yako ya sasa na upo kwenye ngazi ya uongozi, epuka kujilimbikizia sifa zote za ufanisi wa timu yako. Badala yake hakikisha unautambua mchango mkubwa wa timu nzima, na kutambua pia kwa jinsi gani kupitia vipaji vya watu kwenye timu yako, mikakati uliyoiweka imeweza kufanikiwa. Viongozi bora walio wengi wanajua kuwa mafanikio yao yanapimwa kwa ufanisi wa timu wanazoziongoza. Ukiweza kulionesha hili kwenye usaili utafanikiwa kirahisi.
6. ‘Sera yenu ya likizo inasemaje?’
Swali la namna hii linaonesha kuwa tayari unataka mapumziko katika siku yako ya kwanza ya usaili. Waajiri wote wanataka wachapakazi hasa ambao wataifanya kampuni yao kuwa imara zaidi, hawataki watu wanaowaza kwenda mapumzikoni siku yao ya kwanza.
7. ‘Samahani, huwa nachelewa mara kadhaa’
Unapoulizwa kuhusu udhaifu wako kwenye usaili wa kazi, si vyema hata kidogo kusema kuwa una tabia ya kuchelewa kazini. Mtu yeyote ambaye hana hulka ya kutokea sehemu katika muda uliokubaliwa au mapema zaidi si mtu ambaye muajiri anaweza kumuamini na kumuachia ahudumie wateja wake.
8. ‘Kuna wanawake/wanaume wanaovutia kwenye ofisi hii’
Kauli kama hii inaonesha hujakomaa kiakili. Lazima muajiri apate wasiwasi wa tabia yako kutofaa kwenye mazingira ya kazi endapo utapatiwa fursa ya kufanya kazi unayoiomba.
9. ‘Nitakuwa na majukumu gani?’
Mara nyingi, unatakiwa uwe na picha fulani juu ya kazi unayoiomba. Hata hivyo, kama unataka hasa kufanya kazi kwenye kampuni fulani, ni lazima uoneshe kuwa unaweza kufanya kazi unayoiomba na nyinginezo pia.
Swali kama hili linaonesha kuwa utataka kufanya kile tu unachotarajiwa kukifanya, wakati kimsingi majukumu yako ni yale yote utakayotaka kuyafanya. Hasa katika kampuni changa, uwezo wa kufanya kazi mbalimbali huwa inaongeza thamani ya mtu kwa haraka sana.
Unapofanyiwa usaili wa kazi, unaongeza nafasi ya kupata kazi kama utaweza kuonesha utayari au uwezo wako wa kufanya kazi zaidi ya moja.
10. ‘Una wajukuu?’
Hii ni sawa na kumuuliza mwanamke kama ana ujauzito kwakuwa ameona ana tumbo kubwa. Mtu anaweka kuonekana kama anaweza kuwa na wajukuu lakini asiwe nao. Kuwa makini kwa unayoyasema.
11. ‘Mimi ni mtaalamu niliyebobea’
Kuwa makini sana usijisifu kupitiliza.
Badala ya kusema “‘Mimi ni mtaalamu,’ au ‘Nimebobea.’ Sema tu kwamba unavutiwa sana na jambo fulani na kuwa mara kwa mara unapenda kujifunza kuhusu jambo hilo.”
12. ‘Kasoro yangu pekee ni kwamba ninafanya kazi kupita kiasi’
Ni jambo linalowakera waajiri wengi pale wanapouliza kuhusu madhaifu yako na kukuta ukitoa jibu ambalo ni chanya kupita kiasi. Muajiri anahitaji akujue vizuri na wanaelewa kuwa kila mtu ana udhaifu wake, kwahiyo unatakiwa ujue mapungufu yako na uweze kuyasema ili kumuwezesha muajiri kujua atakusaidiaje unapokuwa kazini.
13. ‘Sina swali lolote’
Muombaji anayesema ‘sina swali lolote’ kimsingi ni mtu ambaye aidha hajavutiwa na kampuni yako, majukumu atakayofanya, au bila shaka vyote kwa pamoja.
0 comments:
Post a Comment